Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine jana wameshiriki katika mjadala wa wajumbe kutoka mkoa wa Fujian wanahudhuria mkutano wa Bunge la Umma la China unaoendelea hapa Beijing.
Kwenye mjadala huo, Rais Xi amesisitiza kuwa, inapaswa kuweka mazingira mazuri ya kusaidia sekta ya uvumbuzi na ujasiriamali ili kuzidi kuongeza ushawishi na uwezo wa ushindani wa China katika mchakato wa mabadiliko ya utaratibu wa dunia. Amesema inapaswa kutekeleza sera na hatua mbalimbali katika kuelekeza na kuunga mkono maendeleo ya uchumi wa sekta binafsi. Pia kuonesha sifa ya mkoa wa Fujian, likiwa eneo maalumu la kiuchumi, eneo la majaribio ya biashara huria, eneo la majaribio shirikishi, na eneo muhimu la Njia ya Hariri Baharini ya Karne 21, na kuongeza uwezo wa ushindani wa viwanda mkoani humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |