• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutekeleza kwa hatua zenye ufanisi mipango ya kulinda mazingira mazuri ya hewa

    (GMT+08:00) 2019-03-11 19:16:35

    Waziri wa mazingira na ikolojia wa China Bw. Li Ganjie amesema, wizara yake itachukua hatua thabiti katika kulinda mazingira mazuri ya hewa.

    Bw. Li amesema China imemaliza kutunga sera na mipango kuhusu kulinda mazingira mazuri ya hewa, utaratibu wa kushughulikia suala hilo umeundwa kimsingi, huku kazi ya kupunguza utoaji wa hewa chafu ikiendelea kwa utaratibu.

    Ameongeza kuwa kipaumbele cha sekta hiyo ni kufanya utekelezaji kwa hatua zenye ufanisi, ili kupunguza kwa udhahiri kiwango cha uchafuzi wa vumbi aina ya PM2.5 na idadi ya siku zenye kiwango cha juu cha uchafuzi wa hewa, huku ubora wa mazingira ya hewa ukiboreshwa kwa kiasi kikubwa, ili kuongeza neema ya wananchi kutokana na hewa safi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako