• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Usalama wa ndege aina ya Boeing 737 Max 8 watiliwa shaka

  (GMT+08:00) 2019-03-11 20:36:48

  Ndege ya Boeng huenda ikaathirika kibiashara baada ya usalama wake kuanza kutiliwa shaka kufuatia kuanguka kwa ndege ya shirika la ndge la Ethiopia na kusababisha vifo vya watu 157. Huku uchunguzi ukianzishwa kuhusu ajali ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Addis Ababa, Ethiopia kuelekea Nairobi Jumapili, maswali yameibuka upya kuhusu usalama wa aina hiyo ya ndege ya Boeing 737 MAX 8.

  Mwaka 2018, ndege aina hiyo hiyo ilianguka baharini mnamo Oktoba na kusababisha vifo vya watu wote 189 nchini Indonesia, dakika 13 pekee baada ya kupaa angani.

  Ingawa kumekuwepo na mamia ya ajali za ndege za Boeing tangu miaka ya sabini, ajali hizi mbili zinasababisha wasiwasi kwa kuwa 737 MAX 8 ni kati ya aina mpya zaidi za ndege za Boeing tangu zizunduliwa 2016.

  Ethiopia ilikuwa imepokea ndege yake Novemba mwaka uliopita kutoka kampuni ya Boeing ya Amerika.

  Jana, kampuni hiyo ilisema imejitolea kutoa usaidizi kwa shirika la ndege la Ethiopian Airlines endapo itahitajika kufanya hivyo.

  Ndege hiyo huwa na uwezo wa kubeba abiria kati ya 162 na 210. Ina urefu wa futi 129 inchi nane kwenda nyuma, na futi 40 inchi nne kwenda juu. Mbawa zake ni futi 117 inchi 10 kila moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako