Klabu hiyo imeamua kumtupia virago aliyekuwa akiinoa timu hiyo Santiago Solari baada ya kushindwa kuleta mafanikio kwa klabu hiyo tangu alipotwaa mikoba.
Akiongea na waandishi wa habari, Zidane amesema amerudi Madrid kwasababu rais amemuita na anafuraha kurudi na kuahidi timu inafanya vizuri kwakuwa watu wengi wanaipenda.
Zidane alishahusishwa na mpango wa kujiunga na Chelsea kujaza nafasi ya Maurizio Sarru au Manchester United baada ya kumfukuza Jose Mourinho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |