• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Mazingira la nne lahimiza hatua za kuhifadhi ikolojia

  (GMT+08:00) 2019-03-12 08:05:55

  Washiriki kwenye mkutano wa nne wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEA 4) Mjini Nairobi , wametoa wito wa hatua za haraka za kuhifadhi mazingira ili kuepusha dunia na majanga kama vile mafuriko, uchafuzi wa bahari na ukame.

  Ronald Mutie anaripoti kutoka Nairobi.

  Baraza la Mazingira la nne la Umoja wa Mataifa linawaleta pamoja washiriki 1,700 wakiwamo mawaziri wa mazingira kutoka nchi zaidi ya 170.

  Matokeo ya mkutano huu yatatumika kutoa mwelekeo wa kimataifa na kuongeza uwezekano wa kufanikisha makubaliano ya Paris kuhusu kupunguza uchafuzi wa mazingira na ongezeko la joto duniani.

  Rais wa Mkutano wa UNEA 4 ni waziri wa mazingira wa Estonia bwana Siim Valmar Kiisler .

  "Watu bilioni 2 kote duniani hawana huduma za kukusanya taka kwenye maeneo yao. Watu milioni 64 wanaathiriwa moja kwa moja na uchafuzi au uchomaji wa taka kwenye maeneo ya wazi. Tani milioni 8 za takataka zinaingia kwenye bahari kila mwaka. Hivyo tunahitaji kupunguza sana uzalishaji wa plastiki za matumizi ya mara moja."

  Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa kati ya mwaka 1995 na 2011 dunia imepoteza raslimali za kimazingira za dola trilioni 20.

  Inasema ripoti hiyo kuwa shughuli za kilimo zinagharimu mazingra dola ya trilioni 3 nao uchafuzi ukiletea dunia hasara ya dola ytilioni 4.6 kila mwaka.

  Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano huo Kaimu mkurungezi wa shirika la Umoja la Kulinda mazingira UNEP Bibi Joyce Msuya amesema hali ya sasa inatia hofu.

  "Tusipoangalia swala la uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa basi halijoto itaendelea kuongezeka . Kuna nchi ambazo zinakabiliwa na matatizo mengi ya uchafuzi wa bahari na mazingira kutokana na kuwa na mifumo isiokuwa endelefu wa uchukuzi na viwanda"

  Anasema sasa ni muda wa kuchukua hatua za vitendo kulinda mazingira na kutimiza ahadi ambazo tayari zimetolewa.

  "Mkutano huu wa nne tunatarajia kujitolea na uongozi wa nchi zote kuendana na maudhui ya kukabili changamoto za kimazingira kupitia ubunifu kwenye sekta ya kilimo na utengenezaji bidhaa. Kwa hivyo tunatarajia mawaziri na marais wachache watakaofika, watoke na mpango jinsi gani dunia zima inaweza ikaendeleza maudhui na mkutano wa UNEA 4. "

  Maudhui ya mkutano huu wa hadi Machi 15 ni Ufumbuzi wa ubunifu wa changamoto za mazingira na matumizi na uzalishaji endelevu.

  Na ili kuhimiza kwa kutoa mifano, shirika la Umoja wa mataifa wakati wa mkutano huu, limewaalika wavumbuzi na wajasiriamali wanaowekeza kwenye miradi isiochafua mazingira.

  Bwana Newton Owino anatokea mjini Kisumu ambako anaendesha bishara yake ya kutengeneza viatu kutokana na ngozi ya samaki.

  Anaona hii ni njia yake ndogo ya kuzuia uchafuzi wa ziwa Victoria ambalo ni la pili kwa ukubwa lenye maji safi duniani.

  "Kazi yangu ni kutengeneza bidhaa kama viatu, nguo na mikanda kwa kutumia ngozi ya samaki. Kabla sijaanza hizi ngozi zilikuwa zinatupwa kwa mazingira na hiyo ilikuwa inadhuru afya za watu wenye wanaishi huko"

  Wakati wa mkutano huu pia UNEP itatoa ripoti ya utafiti mpya ikiwa ni pamoja na toleo la hivi karibuni la mazingira kote duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako