Kituo hicho kitakuwa na huduma kama vile mabohari na uongezaji wa ubora kwenye bidhaa.
Aidha kitakuwa na maabara, taasisi ya mafunzo na huduma za kisheria kwa wanawake.
Mwenyekiti wa chama cha wanawake wafanyabishara nchini humo Angela Bageine, amesema kituo hicho kitasaidia wanawake kujinufaisha na fursa za kibiashara na kujikuza kiuchumi.
Fedha hizo zitatoka kwa michango ya wanachama na washirika wengine wanaounga mkono wanawake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |