• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: DTB kufungua taw maalum lenye wahudumu wanawake pekee

    (GMT+08:00) 2019-03-12 19:18:33
    Benki ya DTB nchini Tanzania inakusudia kupata usawa wa kijinsia katika nguvu kazi yake ndani mwaka huu na kufanya mchakato wa kufungua tawi maalum lenye wafanyakazi wanawake jijini Dar es Salaam.

    Meneja Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Teknolojia DTB, Stella Masha, amesema benki hiyo inazingatia usawa na ndio maana wanataka kufungua tawi maalum litakalohudumiwa na wanawake.

    Masha alisema kama ilivyo sera yao ya rasilimali watu benki ya DTB inaunga mkono usawa wa kijinsia katika kutoa ajira na wamefanikiwa kwa asilimia 49.1 ni wanawake.

    Aidha, alisema katika matawi 14 yaliyopo Dar es Salaam asilimia 50 ni wanawake, benki imekusudia kupata usawa wa jinsia katika nguvu kazi yake katika mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako