Meneja Mkuu wa Tanga Fresh, Michael Karata alisema kiwanda hicho kinahitaji lita 120,000 kwa siku lakini mpaka sasa wanasindika lita 50,000 tu.
Alisema, sehemu kubwa ya maziwa wanategemea kutoka kwa wafugaji lakini wameshindwa wameshindwa kukidhi mahitaji ya kiwanda.
Licha ya kuchanganya maziwa na maji, Karata alisema sababu nyingine ni ng'ombe kukosa lishe bora na ukame.
Alisema awali walilazimika kununua maziwa nje ya nchi, lakini kwa sasa hawafanyi hivyo na kwamba licha ya kuongeza vituo vya kukusanyia maziwa kwa baadhi ya mikoa, bado kiasi kinachopatikana hakikidhi mahitaji ya kiwanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |