• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria ya uwekezaji wa kigeni kunufaisha wawekezaji wa nje na wa ndani

    (GMT+08:00) 2019-03-12 19:43:20

    Mswada wa sheria ya uwekezaji wa kigeni umewasilishwa katika Bunge la Umma la China ili kupitiwa.

    Wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya kisiasa la China wanaona kuwa, sheria hiyo si kama tu itaongeza imani ya wawekezaji wa nje kwa mazingira ya biashara ya China, bali pia itanufaisha kampuni binafsi za China.

    Mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya kisiasa la China Bi. Jiang Ying amesema, sheria hiyo itaongeza imani ya wawekezaji wenye wasiwasi kuhusu mazingira ya biashara nchini China, anasema,

    "Sheria hiyo imesisitiza sana uwazi, usawa, uhakikisho na makadirio, na kutoa jibu la moja kwa moja kwa wawekezaji wa nje wenye wasiwasi. Tunatakiwa kuacha vitendo vya kuingilia visivyostahili huku tukitekeleza majukumu yetu kwa makini, licha ya hayo tunapaswa kutoa huduma nzuri."

    Mjumbe mwingine Bw. Liu Wei amesema, kampuni binafsi za China pia zitanufaika na sheria hiyo, kwani itayasaidia kufanya uwekezaji katika nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako