• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vituo vya mafunzo ya ajira vyasaidia watu kutimiza ndoto mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-03-12 20:57:44

    Mwezi Machi si majira ya kitalii mkoani Xinjiang, China, lakini kuna wageni wengi katika sehemu inayouza vyakula vya asili katika mji wa Kashgar kusini mwa mkoa huo. Watu hao kutoka ndani nan je ya nchi wanakula vyakula vitamu huku wakiburudishwa na ngoma ya kabila la Wauyghur.

    Mkuu wa sehemu hiyo Imam Hasan alikuwa na mkahawa mdogo wa tambi tu, na mwezi Novemba mwaka jana alikodisha eneo hilo, na kusema mafanikio yake yanatokana na kituo cha mafunzo ya ajira.

    Kituo hicho kilianzishwa na serikali kwa ajili ya kugeuza mawazo ya watu wenye msimamo mkali na wale waliofanya uhalifu mdogo, na kuwasaidia kupata ujuzi wa kazi.

    Yusuf Mamut ni mwanafunzi katika kituo hicho. Anapokumbuka vitendo vyake kabla ya kuingia katika kituo hicho, anajisikia vibaya sana. Zamani, kutokana na athari ya msimamo mkali wa kidini, alikuwa na chuki sana dhidi ya watu wanaovuta sigara na kunywa pombe, mara kwa mara aliwapiga watu hao ambao baadhi yao hata ni marafiki na wafanyakazi wenzake. Alijua vitendo vyake vimekiuka sheria, hivyo aliposikia kuna kituo cha aina hiyo, alijiunga nacho kwa hiari.

    Mamut alichagua kujifunza utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki. Sasa anapanga kufanya biashara pamoja na rafiki yake Mahmut Memet baada ya kutoka kwenya kituo hicho. Memet pia ni mwanafunzi wa kituo hicho, na anapenda kujifunza lugha sanifu ya kichina, ili kufanya biashara vizuri baadaye.

    Licha ya utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki na lugha ya kichina, kituo hicho pia kinatoa mafunzo ya usanifu wa nguo, biashara kupitia mtandao wa Internet, na ufundi wa kutengeneza tambi ya kikabila.

    Nurli Turgun aliyehitimu chuo kikuu anachukua kituo cha mafunzo ya ajira kama ni nafasi yake ya kusoma tena katika chuo kikuu. Katika kituo hicho, alijifunza lugha ya kichina, sheria, uandishi na usanii.

    Kama hali ilivyo katika chuo kikuu, wanafunzi wa kituo hicho wanapata siku za mapumziko wakati wa wikiendi. Abdukadir Dawut anamtembelea mama yake kila wiki. Mama yake anasema, baada ya kujiunga na kituo cha mafunzo ya ajira, mtoto wake amekuwa na mabadiliko makubwa, na sasa ni mtulivu na anampenda sana. Anaishukuru serikali kwa kumpa Dawut mafunzo mazuri.

    Dawut ana nyumba kubwa ambayo inahitaji ukarabati. Serikali itatoa ruzuku isiyopungua dola 4200 za kimarekani. Mkewe Zohre Memet alisema zamani Dawut alikuwa na msimamo mkali, na kumtendea vibaya sana, ila sasa amebadilisha msimamo, na amekuwa mtulivu sana.

    Ingawa baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi vinasema vituo vya mafunzo ya ajira mkoani Xinjiang ni kama jela, lakini ukweli ni kwamba, vituo hivyo vimewapa watu fursa ya kuboresha maisha yao. Nurbiya Yunisi ni msichana mrembo, atahitimu mafunzo yake katika kituo cha mafunzo ya ajira. Ana ndoto ya kuanzisha duka la nguo, na kuwa bosi mkubwa. Anasema kituo hicho ni kizuri sana, na kimemfundisha ufundi wa kutengeneza nguo.

    Msimamo mkali na ugaidi ni tishio linaloikabili dunia nzima, na nchi nyingi zinatafuta njia ya kulitatua kutokana na hali yao tofauti. Sehemu ya kusini mwa mkoa wa Xinjiang ambayo inaathiriwa vibaya na msimamo mkali wa kidini ilikumbwa na mashambulizi ya kigaidi mara nyingi. Katika sehemu hiyo, vituo vya mafunzo ya ajira vinawasaidia watu kuondokana na msimamo mkali, na vimekuwa njia ya uvumbuzi ya kukabiliana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako