• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FKF na Harambee Stars wapata mdhamini wa Kampuni ya Betin

    (GMT+08:00) 2019-03-13 08:19:50
    Kuelekea mashindano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON 2019), timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imepata mdhamini mpya atakayesimamia gharama zote za timu hiyo.

    Kwenye dili hilo la mwaka mmoja lililosainiwa jana, kampuni ya kubeti ya Betin imeingia mkataba huo wa shilingi milioni 20 na shirikisho la soka la Kenya (FKF), dili ambayo itagharamia maandalizi ya timu hiyo, gharama ya jezi za timu na za mashabiki.

    Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, rais wa FKF Nick Mwendwa amesema udhamini huo utasaidia kuwezesha kambi ya Harambee Stars ambayo imepangwa kuwa nchini Ufaransa wiki tatu kabla ya kuelekea Misri.

    Harambee stars inayoongoza kundi D itaondoka nchini Kenya Machi 22 kuelekea jijini Kumasi Ghana kwa ajili ya mechi ya mwisho ya kundi hilo kufuzu AFCON.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako