• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa Brexit wa Waziri mkuu wa Uingereza wakataliwa tena bungeni

    (GMT+08:00) 2019-03-13 09:13:39

    Mpango mpya wa makubaliano ya Brexit uliowasilishwa jana kwenye baraza la makabwela la Bunge la Uingereza na waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May, umekataliwa na kufanya hali ya sintofahamu kuhusu jinsi Uingereza itakavyojitoa Umoja wa Ulaya.

    Hii ni mara ya pili tangu januari 15 kwa wabunge kukataa mpango wa Brexit, safari hii wamekataa kwa kura 391 dhidi ya 242. Juhudi za mwisho za Bibi May kupata uungaji mkono wa makubaliano yake zilishindwa kuvutia uungaji mkono wa chama cha Leba na kundi la ERG ndani ya chama chake cha wahafidhina.

    Baada ya upigaji kura Bibi May amesema amesikitishwa na matokeo ya upigaji kura huo, na kusema Uingereza sasa inakabiliwa na chaguo gumu.

    Upigaji kura wa pili unatarajiwa kufanyika leo ili kuepusha Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya bila makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako