• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa CPPCC wamalizika Beijing

    (GMT+08:00) 2019-03-13 10:34:51

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC, ambalo ni chombo cha juu cha kutoa ushauri wa kisiasa nchini China, umemalizika leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa chama na serikali wamehudhuria ufungaji wa mkutano huo.

    Mwenyekiti wa CPPCC Bw. Wang Yang ametoa hotuba akisema huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Katika kipindi hicho, CPPCC imejitolea katika kuanzisha Jamhuri ya Watu wa China, kuijenga China, kutafuta njia ya mageuzi na kutimiza ndoto ya China. Amesema ujamaa wenye umaalumu wa kichina umeingia kwenye zama mpya na majukwaa ya CPPCC yatakuwa mapana zaidi, na majukumu yatakuwa makubwa zaidi. Ameitaka CPPCC ishikilie kithabiti nafasi yake, kutumia kwa usahihi mkondo wa kihistoria na kusukuma mbele maendeleo ya CPPCC.

    Mkutano wa pili wa Kamati ya Taifa ya 13 ya CPPCC umefanyika kwa siku 11 zilizopita, na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 2,100 kutoka vyama, makundi na makabila mbalimbali kote nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako