• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo kuhusu utamaduni na michezo barani Afrika yafuatilia ushirikiano wa michezo kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-03-13 17:05:41

    Mashindano ya soka ya wanaume ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja yatafanyika mwezi Juni mwaka huu nchini Misri. Ili kutumia fursa hii kuhimiza ushirikiano wa michezo kati ya China na Afrika, mazungumzo kuhusu utamaduni na michezo barani Afrika yalifanyika jana mjini Cairo, Misri.

    Madhumuni ya kufanya mazungumzo kuhusu utamaduni na michezo barani Afrika ni kujadili mpango wa ushirikiano wa makampuni ya China katika soko la michezo barani Afrika. Mazungumzo hayo yamemshirikisha konsela wa ubalozi wa China nchini Misri anayeshughulikia mambo ya biashara Bw. Han Bing, maofisa wa juu wa shirikisho la soka la Misri, wajumbe wa makampuni ya China nchini Misri, na wajumbe wengine wa China na wa nchi nyingine.

    Alipohutubia mazungumzo hayo, Bw. Han amesema ikiwa sehemu muhimu ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", mawasiliano ya michezo na utamaduni yanafanya kazi muhimu katika kuhimiza mawasiliano ya kimataifa ya ustaarabu. Ameongeza kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika ni mashindano muhimu zaidi ya soka barani Afrika, makampuni ya China yanapaswa kutumia fursa hii kuhimiza zaidi mawasiliano na ushirikiano barani humo. Anasema,

    "Misri itakuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na hii pia ni changamoto kwa nchi hiyo. Lakini tumetambua kasi ya maendeleo ya nchi hiyo. Hivyo changamoto hiyo pia ni fursa nzuri kwa Misri, na pia ni fursa kwa makampuni ya China nchini humo."

    Soka ni moja kati ya michezo inayopendwa zaidi na waafrika. Utamaduni maalumu wa kisoka wa Afrika pia unafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa. Shirika la Lagardere Sports la Ufaransa ni mwenzi pekee wa Shirikisho la Soka la Afrika, katika shughuli za uenezi na masoko. Kwenye mazungumzo hayo, limepongeza makampuni ya China kwa mchango wao nchini Misri na kote barani Afrika, na kutumai makampuni hayo yatasaidia Afrika kuendeleza soko la mchezo wa soka.

    Bw. Mohamed Fadl aliyekuwa nyota wa soka wa Misri ni msimamizi mkuu wa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Alipozungumzia maandalizi ya mashindano hayo, Bw. Fadl ameeleza matarajio yake ya kufanya ushirikiano na makampuni ya China. Amesema Misri ina uwezo mbalimbali wa kuandaa mashindano hayo, lakini makampuni ya China yanaweza kutoa misaada inayohitajika. Anasema,

    "Soka ni lugha ya pamoja ya binadamu isiyo na mipaka. Soko la soka la Misri linapanulika kwa kiasi kikubwa. Idadi kubwa ya mashabiki na uzoefu mkubwa wa kuandaa mashindano makubwa ni mategemeo yetu ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika tena. Tume yetu ya maandalizi itafanya vizuri shughuli za ugavi, ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, usafirishaji na huduma za afya. China ni moja ya nchi kubwa zaidi kwa ukubwa wa uchumi duniani, Misri inatilia maanani ushirikiano kati yake na makampuni ya China katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako