Mkutano wa Pili wa Bunge la awamu ya 13 la Umma la China utajadili na kupiga kura kuhusu Mswada wa Sheria ya uwekezaji wa kigeni, ambao ni moja kati ya ajenda muhimu katika mkutano huo.
Ikiwa ni sheria mpya ya kimsingi katika sekta ya uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni nchini China, sheria hiyo imeweka kanuni za pamoja kuhusu kuidhinisha, kuhimiza, kulinda na kusimamia uwekezaji wa kigeni. Wajumbe wa bunge la umma la China wameeleza kuwa, sheria hiyo itatoa hakikisho thabiti kwa ufunguaji mlango wenye kiwango cha juu zaidi.
Mjumbe wa Bunge la Umma la China Bibi Zheng Shuna amesema, kujadili na kupiga kura sheria ya uwekezaji wa kigeni kuna umuhimu mkubwa wa kihistoria. Hatua ya utungaji wa sheria hiyo imeonesha jinsi Bunge la Umma la China na kamati zake zinavyoshikilia kutunga sheria kwa njia za kisayansi, kidemokrasia na kufuata sheria, pia imejumuisha uzoefu wa China katika kuvutia uwekezaji wa kigeni kwa njia ya kufungua mlango katika miaka 40 iliyopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |