• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa wito wa kuhimiza mazungumzo ya kisiasa na kuunga mkono uchaguzi wa urais Afghanistan

    (GMT+08:00) 2019-03-13 19:27:34

    Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao ametoa wito wa kuhimiza mazungumzo ya kisiasa nchini Afghanistan na kuunga mkono uchaguzi wa urais nchini humo.

    Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Afghanistan hapo jana, balozi Wu amesema kutimiza amani na maendeleo ya kudumu nchini Afghanistan kunahusiana na maslahi ya raia wa nchi hiyo pamoja na usalama, utulivu, maendeleo na ustawi wa kikanda. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kutekeleza ahadi zake na kuendelea kuiunga mkono kithabiti Afghanistan.

    Ameongeza kuwa Afghanistan itafanya uchaguzi wa urais ndani ya mwaka huu, na kuitaka tume huru ya uchaguzi nchini humo iimarishe kazi ya maandalizi, vyama vyote nchini humo vinapaswa kushikamana zaidi na kulinda utulivu wa taifa, na kutatua masuala kwa njia ya mazungumzo. China inapenda kutoa mchango wake kwa ajili ya usalama, utulivu, maendeleo na ustawi nchini Afghanistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako