• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China azungumza na wajumbe wa Bunge la Umma la China kutoka ngazi ya shina

    (GMT+08:00) 2019-03-13 19:32:31

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na wajumbe kutoka mikoa ya Mongolia ya Ndani, Henan, Fujian,na Gansu wanaohudhuria mkutano wa Bunge la Umma la China, na kusikiliza maoni yao kuhusu masuala mbalimbali.

    Baada ya kusikiliza maoni ya wajumbe hao, rais Xi amesisitiza kuwa ni lazima kuimarisha ujenzi wa kulinda mazingira ya ikolojia, na haipaswi kukuza ongezeko la uchumi kwa kuharibu mazingira. Amesema kuhakikisha utoaji wa mazao ya kilimo hususan vyakula ni kipaumbele muhimu kwa utekelezaji wa mikakati ya kustawisha vijiji, na kuzingatia ujenzi wa miundombinu vijijini, kukamilisha utaratibu wa bima ya utunzaji wa wazee mijini na vijijini pia ni muhimu. Rais Xi amesisitiza kuwa, ni muhimu kukamilisha utaratibu wa uhakikisho wa kima cha chini cha maisha, kukamilisha utaratibu wa utunzaji wa watoto ambao wazazi wao wanatafuta vibarua vijijini, pamoja na wanawake na wazee vijijini.

    Ameongeza kuwa kando mbili za mlango bahari wa Taiwan zinapaswa kuwasiliana, na inapaswa kusikiliza mahitaji ya wakazi wa Taiwan, na kutafuta sera na njia za kuwanufaisha. Pia amesisitiza kuwa ni lazima kutekeleza kazi mbalimbali hadi lengo la kuondoa umaskini litakapotimia kabla ya mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako