• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yaongeza bajeti yake kwa shilling bilioni 600

  (GMT+08:00) 2019-03-13 19:39:20

  Tanzania imepanga kuongeza bajeti yake kwa Sh600 bilioni tu kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

  Bajeti ya mwaka unaoishia Juni 30 ilikuwa Sh32.5 trilioni, lakini ya mwaka ujao imepanga kufikia Sh33.1 trilioni.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametoa takwimu hizo wakati akiwasilisha kwa wabunge Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ukomo wa bajeti kwa mwaka 2019/2020.

  Lakini kati ya fedha hizo, Serikali inatarajia kukusanya Sh23 trilioni kutoka katika mapato ya ndani yakijumuisha halmashauri, wakati nakisi itajazwa na fedha nyingine zitakazotokana na wafadhili, mikopo nafuu na ya masharti.

  Hii ni mara ya nne kwa Serikali ya Magufuli kusoma ukomo wa bajeti yake. Katika makadirio yake ya mwaka 2016/17 ilipanga bajeti ya Sh29.5 trilioni, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya Sh7 trilioni ya bajeti iliyoachwa na Serikali ya Awamu ya Nne.

  Kwa mikakati ya 2019/20, mapato ya Serikali yanatarajiwa kuwa Sh22.2 trilioni na kati ya hizo zinazotokana na kodi ni Sh19.1 trilioni na mapato yasiyo ya kodi ni Sh3.1 trilioni, wakati mapato ya halmashauri yanatarajiwa kuwa Sh765.4 bilioni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako