• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za Ufaranza zazozania tenda ya ujenzi wa barabara

    (GMT+08:00) 2019-03-13 19:39:44

    Kampuni mbili za ujenzi za Ufaransa zinapigania kandarasi ya shilingi bilioni 180 ya ujenzi wa barabara ya Nairobi hadi Nakuru. Mamlaka ya ujenzi wa barabara nchini Kenya KENHA imeichagua kampuni ya Rift Valley Connect ambayo inajumuisha kampuni za Vinci Highways SAS, Meridian Infrastructure Africa Fund and Vinci Concession SAS. Hata hivyo kamati ya kutatua migogoro wa tenda imepokea malalamiko kutoka kwa kampuni zingine zikidai kulikuwa na upendeleo.

    Kampuni hizo zinasema KENHA haijatoa sababu za kutochaguliwa kwao kwa kandarasi hiyo. Mgogoro huo unakuja wakati ambapo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kuwasili hii leo nchini Kenya kwa ziara ya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako