• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATCL yasaini mkataba wa kibiashara na kampuni ya China TIHG

    (GMT+08:00) 2019-03-13 19:40:03
    Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) na Kampuni ya Touchroad International Holdings Group (TIHG) ya nchini China wamesaini mkataba wa kuingia kwenye maongezi ya kibiashara ya namna ya kuwasafirisha watalii zaidi ya 10,000 wanaotarajia kuingia nchini Tanzania kwa mwaka 2019.

    Awali, TIHG ilisaini mkataba na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ya kuleta watalii hao 10,000 mwaka jana kwa kutumia ndege zake, hivyo utiaji saini wa mkataba huo na ATCL ni mwendelezo wa kuanza kwa utekelezaji wake ambapo kampuni hiyo italeta hapa nchini watalii kutoka China kisha watalii hao watatumia ndege za ATCL kuelekea maeneo mbalimbali ya utalii nchini.

    Akizungumza na Radio China, Mwenyekiti wa TTB, Jaji Thomas Mihayo amesema katika kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa na mchango mkubwa katika uchumi, imeanza kutekeleza makubaliano ya kuleta watalii 10,000 nchini humo.

    Kwa upande wake, meneja mauzo na usambazaji wa ATCL, Edward Mkwabi amesema shirika hilo limejipanga kufanya kazi hiyo ya kubeba watalii na kwamba makubaliano yaliyofanyika ni ya kuingia kwenye mawasiliano ya namna gani biashara itafanyika.

    Naye, Mwenyekiti wa Kampuni ya TIHG, He Liehu amesema kampuni hiyo pia imejipanga vyema kufanya biashara ya kuleta watalii nchini humo kupitia ndege zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako