• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CRBC yapendekezwa kwa tenda ya kukarabati reli za katikati ya Jiji la Nairobi

  (GMT+08:00) 2019-03-13 19:40:30
  Kampuni ya China ambayo ilihusika na ujenzi wa reli ya wastan SGR CRBC imepata kazi nyingine ya kukarabati reli ya kutoa huduma za usafiri katikati ya jiji la Nairobi .Waziri wa usafiri wa Kenya Bw James Macharia amelitaka baraza la mawaziri kuidhinisha chaguo hilo bila kuiingiza kampuni hiyo kwenye ushindani wa kupigania tenda hiyo.

  Macharia amesema CRBC ni kampuni ambayo imeonyesha uwezo wake na ana imani kuwa itafanya kazi nzuri. Serikali tayari imeagiza injini za treni za dizeli kwa gharama ya shilingi bilioni 1.5 kutoka nchini Huispania. Injini hizo zitaunganishiwa mabehewa na kuanza kutoa huduma za usafiri kwa wenyeji wa jiji la Nairobi na viunga vyake. Reli ya sasa imezeeka na ina kasi ya chini ya kilomita 15 kwa saa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako