• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujumbe wa China waeleza mafanikio katika haki za binadamu mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-03-14 17:13:04

    Ujumbe wa China unaohudhuria hafla ya Umoja wa Mataifa umewafahamisha wanadiplomasia wa kigeni na wajumbe wengine kuhusu mafanikio ya kuboresha haki za binadamu katika mkoa unaojiendesha wa Xinjian Uygur.

    Akizungumza kwenye hafla hiyo, Kiongozi wa ujumbe wa China kwenye ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Yu Jianhua amesema, Xinjiang inafurahia maendeleo ya kasi na utulivu zaidi kuliko siku za nyuma, na makabila yote katika eneo hilo yanapewa ulinzi kamili wa haki zao za kiuchumi, kisiasa, kijamii, kitamaduni, na kimazingira.

    Hafla hiyo ni sehemu ya mkutano wa 40 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini Geneva.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako