• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Taasisi za TPA,TRA,na TRC zatajwa kuchangia ucheleweshaji mizigo bandarini

    (GMT+08:00) 2019-03-14 19:40:09
    Waziri wa ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania,Isaac Kamweli amesema haridhishwi na operesheni za bandari kwa kuwa kuna taasisi tatu ambazo zinachangia ucheleweshwaji wa mizigo ya ndani na nje ya nchi.

    Kamwele alizitaja taasisi hizo kuwa ni Mamlaka ya Bandari (TPA),Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),na Shirika la Reli Tanzania (TRC).

    Kamwele aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya Shirika la Reli Tanzania na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wa kukarabati mabehewa 40 ambayo yatagharimu $600,000 sawa na Tsh1.13 bilioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako