• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-Wajasiriamali wadogo wahimizwa kushirikiana kabla ya uzalishaji wa mafuta kuanza

  (GMT+08:00) 2019-03-14 19:40:28
  Wajasiriamali wadogo na wa kati wamehimizwa kutumia fursa zilizoko katika sekta ya mafuta na gesi kwa kuanzisha ushirikiano ambao utatoa huduma zinazohitajika.

  Haya ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Migodi cha Uganda,Dk Elly Kuruhanga.

  Akizungumza katika kongamano la wajasiriamali la Stanbic jijini Kampala jana.Dk Kuruhanga alisema wenye biashara ndogo na za kati wanafaa kushirikiana ili wawe na uwezo kabla ya uzalishaji wa mafuta ya biashara unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

  Kulingana na wataalamu,ubia au ushirikiano,utarahisisha uwekezaji katika sekta hiyo inayohitaji mtaji kubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako