• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Wafanyabiashara wa samaki jijini Mwanza walia kuongezwa kwa ushuru

    (GMT+08:00) 2019-03-14 19:40:46
    Wanunuzi wa samaki aina ya sangara ,katika halmashauri ya Buchosa,Sengerema,mkoani Mwanza,wameilalamikia halmashauri hiyo kwa kuwatoza ushuru wa Sh.200 kwa kila kilo moja.

    Mwenyekiti wa Umoja wa Wanunuzi wa samaki hao ,Gregory Kazimbo jana alisema kuwa suhuru huo ni mkubwa kwa sababu kwenye mialo wanalazimika kununua kwa Sh3,500 kwa kilo na kuuza viwandani kwa Sh4,000.

    Alisema wamepeleka maombi yao katika halmashauri ya baraza la madiwani liwasaidie kubadilisha ushuru huo mkubwa hadi angalau Sh30.

    Aliongeza kuwa awali walikuwa wakilipa ushuru wa jumla kwa kila safari moja ambayo ilikuwa Sh100,000 lakini sasa umebadilika jambo ambalo linawaumiza katika biashara yao na kuwakosesha faida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako