• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: JPM akabidhiwa ramani ya uwanja mpya wa soka utakaojengwa Dodoma

  (GMT+08:00) 2019-03-15 07:50:55

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na wataalamu wa ujenzi wa uwanja wa soka toka nchini Morocco na kukabidhiwa ramani ya uwanja huo wa kisasa wa mpira utakaojengwa Jijini Dodoma.

  Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Abdelillah Benry.

  Uwanja huo unatarajia kujengwa eneo la Nara Jijini Dodoma, barabara ya kuelekea Singida ambapo jumla ya hekari 143 zimetengwa. Unatarajia kugharimu Tsh bilioni 56 na ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 85,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako