• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China kuwa nanga ya kudumisha utulivu wa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2019-03-15 12:11:55

    Uchumi wa China unatarajiwa kuwa nanga ya kudumisha utulivu wa uchumi wa dunia siku zote.

    Hayo yamesemwa leo na Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alipokutana na waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya China akisisitiza kuwa China itajitahidi kuchochea uchangamfu wa soko, na ikifanikiwa kuamsha hamu ya kufanya uvumbuzi, hakika itaweza kudumisha ukuaji wa uchumi kwa kasi inayofaa, na kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu.

    Bw. Li amesema China inakabiliwa na changamoto mpya ya kiuchumi, lakini kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia nzima inapungua, na katika mwezi uliopita mashirika mengi makuu ya kimataifa yalipunguza makadirio yao kuhusu ukuaji wa uchumi wa dunia. Ameongeza kuwa China ina mbinu mbalimbali za kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha nakisi, na kupunguza kiwango cha riba na akiba ya lazima ya benki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako