Waziri mkuu wa China Bw. Li keqiang leo amesema, mwaka huu serikali ya China itaendelea kutoa orodha mpya ya sekta zisizoruhusu wafanyabiashara wa nchi za nje kuwekeza, kuendelea kuimarisha ulinzi wa hakimiliki, na kuidumisha China kufungua mlango.
Bw. Li Keqiang amesema, China imetekeleza utaratibu wa orodha ya sekta zisizoruhusu wafanyabiashara wa nchi za nje kuwekeza na kuwatendea wafanyabiashara wa nchi za nje sawa na wa ndani. Mwaka huu China itatoa orodha hiyo mpya, na kupunguza sekta zisizoruhusu wafanyabiashara kuwekeza. Vilevile, China itarekebisha sheria ya hakimiliki za ubunifu.
Amesema kuwa, mkutano wa pili wa awamu ya 13 wa bunge la umma la China umepitisha sheria ya uwekezaji wa nchi za nje, hii imeonyesha kuwa China itatumia njia ya kisheria kulinda uwekezaji wa nchi za nje, na kuvutia uwekezaji kutoka nje.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |