Uchina unatarajia matakeo bora kwenye mazugumzo yao na Marekani kuhusu ushirikiana wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili unayo endelea, waziri mkuu Li Keqiang atangaza siku ya Ijumaa.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya bunge la kitaifa kufungwa rasmi, bwana Li alisisitiza kuwa Uchina ina matumaini kuwa mashauriano unayo endelea baina yao na Marekani itazaa matunda ya faida kwa pande zote.
"Kama serikali, tunatuwai kuwa matokeon ya mazungumzo yetu itafaidi pande zote na ulimwengu mzima utafurahia tendo hilo," asema bwana waziri mkuu.
Aliongezea kuwa historia ya Uchina na Marekani umetoka mbali na uchumi wan nchi hizo mbili unategemeana kwa hivyo hakuna vile pande moja unaezaacha kuhusisha pande ingine.
"Sisi kama wachina, tunaamini kuwa tutaendelea kufuata kanuni za ushirikiana badala ya kukorofishiana kwa ajili ya kuheshimiana na usawa ili kukuza uchumi ya ulimwengu," kasema bwana Li.
Alifahamisha dunia kuwa serikali ya Xi Jinping haitahusisha nchi zingine kwenye vita vyao vya kibiashara na Marekani.
Bwana Li asisitiza kuwa serikali ya Uchina china ya mwokozo wa Rais Jinping unafanya wawezalo ili kukuza uchumi wa nchi hilo na kuhakikisha wanabiashara kuwa wasikuwe na wasiwasi.
Huu na baada ya wabunge kupitisha ule mswada wa sharia ya uwekezaji ya nje ambayo itawawezesha wawekezaji kutoka nchi mbali mbali kuwa na uhuru wa kutuma faida wanazopata kutoka kwa biashara zao nchini Uchina kwa nchi za.
Sheria hiyo ambayo itaanza kufanya kazi Januari mosi, 2020 inazuia serikali ya Uchina kuingilia biashara za wageni na inalinda wenye biashara kutodhulumiwa kwa njia ya kuwalazimisha kuhamisha teknolojia zao kwa seikali.
"Serikali inajukumu sasa kuunda taratibu na kanuni tofauti tofauti ili zipige jeki sheria ya uwekezaji ya nje kwa miundo msingi wa kulinda wanabiashara kutoka nchi za nje," bwana Li atangaza.
Wadadisi wa kiuchumi wanakisia kuwa Uchina unapanga kutumia sheria uliyopitishwa siku ya Ijumaa ili kuwavutia Marekani kwa msingi wa kuona kuwa ushirikiano wa nchi hizo mbili ufanikiwe.
Bwana Li amesema kuwa kuwa serikali ya rais Xi itaendelea kukabiliana na janga la umaskini kwa kuhakikisha kuwa wanaomaliza masomo ya chuo kikuu wamepata kazi akisimulia kuwa wengi wao ni tegemeo katika familia wanaotoka.
"Mwaka huu tunakisia kuwa karibu wanafunzi millioni nane nukta mbili watahitimu kutoka vyuo mbali mbali na kwa sababu serikali ya rais Xi inakabiliana na janga la umaskini, tutatenga nafasi za ajira millioni kumi na moja mwaka huu kama njia moja wapo wa kumaliza umaskini ufikiapo mwaka ujao," asema waziri mkuu.
Aliezakuwa kuwa wamepitia changamoto chungu msima kudhibiti uchumi wa nchi na wako na imani kuwa pato la nchi ya asilimia sita nukta tano itafikishwa mwaka huu.
"Tumepanga kama serikali kuwa pato la nchi mwaka huu itakuwa asilimia 6.5 na tunamatumaini kuwa tutafanikiwa ijapokuwa tutapitia mengi tena mwaka huu kwa ya uchumi," akasema.
Uchina ni nchi ya pili baada ya Marekani kuwa na uchumi bora ulimwenguni na wakati uchumi wake unaonekana kama kwamba inazoroteka, inaleta wasiwasi mwingi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |