• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China aonesha imani kubwa kuhusu uchumi wa China katika siku za baadaye

    (GMT+08:00) 2019-03-15 18:52:20

    Mkutano wa Pili wa Bunge la Awamu ya 13 la Umma la China uliofungwa leo mjini Beijing umepitisha ripoti ya kazi ya serikali ya awamu hiyo, na sheria ya uwekezaji wa kigeni inayolenga kuhimiza ufunguaji mlango katika kiwango cha juu zaidi. Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya kumaliza kwa mkutano huo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameeleza kuwa, China itafuata hali ilivyo hivi sasa, kutupia macho siku za baadaye, kudumisha ongezeko lenye utulivu la uchumi na mwelekeo mzuri wa ongezeko hilo. Anaamini kuwa uchumi wa China utakuwa msukumo muhimu katika uchumi wa dunia.

    Akizungumzia hali ya uchumi nchini China kwa mwaka huu Bw. Li Keqiang anasema:

    "Uchumi wa China kweli unakabiliwa na changamoto mbalimbali. Hivi sasa kasi ya ongezeko la uchumi duniani imepungua, katika mwezi mmoja uliopita, mashirika makubwa ya kimataifa yenye ushawishi mkubwa yamepunguza makadirio ya ongezeko la uchumi duniani. China pia imepunguza kwa kiasi lengo la makadirio hayo hadi katika kiwango kinacholingana na ongezeko la uchumi la mwaka jana, na wala haitafanya uchumi kuzorota chini ya kiwango kinachofaa."

    Sheria ya uwekezaji wa kigeni iliyopitishwa kwa kupigiwa kura itatekelezwa rasmi kuanzia tarehe 1 Januari, mwaka kesho. Bw. Li Keqiang ameeleza kuwa, sheria hiyo si kama tu italinda na kuvutia uwekezaji wa kigeni, bali pia itaweka nidhamu na sheria kwa uendeshaji wa serikali. Anasema:

    "Serikali itatunga kanuni na nyaraka mbalimbali kwa kufuata sheria hiyo, ili kulinda maslahi ya wafanyabiashara wa kigeni. Vilevile tutaimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu, kurekebisha hakimiliki ya ubunifu, na kuadhibu vibaya vitendo vya kukiuka hakimiliki ya ubunifu."

    Akizungumzia mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, Bw. Li Keqiang ameeleza kuwa mwelekeo wa uhusiano kati ya pande hizo mbili wa kupata maendeleo haubadiliki, kwa sababu maslahi ya pamoja kati ya pande hizo mbili ni mengi zaidi kuliko mikwaruzano iliyopo kati yao. Anasema:

    "Mazungumzo kati ya China na Marekani kuhusu migogoro ya biashara kati yao bado yanaendelea. Tunatumaini kuwa mazungumzo hayo yatapata matokeo mazuri na kuzinufaisha pande zote mbili. Pia tunaamini kuwa wananchi wa China na Marekani wana busara na uwezo wa kudhibiti na kutatua migogoro na tofauti zilizopo kati yao, na kuhimiza uhusiano kati ya pande mbili kupata utulivu na maendeleo mazuri."

    Pia amesisitiza kuwa mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani unahusisha pande hizo mbili tu, China haitatumia upande wa tatu wala kuharibu maslahi ya upande wa tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako