• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TFDA yasema ulaji wa vyakula vilivyochafyliwa na sumukuvu huleta madhara kwa afya

  (GMT+08:00) 2019-03-15 19:28:46

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema ulaji wa vyakula vilivyochafuliwa na kiasi kikubwa cha sumukuvu husababisha madhara ya kiafya ya muda mfupi na muda mrefu.

  Madhara ambayo mtu anaweza kuyagundua baada ya muda mrefu kupita ni ya kuugua saratani ya ini na madhara ya muda mfupi ni mlaji kuugua ugonjwa wa kuhara.

  Sumu hiyo hupatikana kwenye mazao ya nafaka hasa mahindi na karanga, na kwamba walaji wa ugali wa dona wapo hatarini zaidi ikiwa hatua za uandaaji wa chakula hicho hautazingatiwa.

  Hayo yalizungumzwa jana na msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwaza alipoulizwa kuhusu hatua zinazochukuliwa kudhibiti waandaaji wa unga wa dona nchini humo na madhara yanayoweza kumpata mtu endapo atakula chakula hasa ugali wa dona ambayo imechafuliwa na sumu kuvu.

  TFDA imekuwa ikitoa maelekezo kwa wamiliki wa viwanda vyenye mashine na watu mbalimbali kuhusu hatari hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako