• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sekta ya mifugo Tanzania yachangia asilimia 6.9 ya pato la taifa

  (GMT+08:00) 2019-03-15 19:29:27

  Sekta ya mifugo nchini Tanzania inasemekana kuchangia asilimia 6.9 ya pato la Taifa, wakati viwango vya kimataifa ni kufikia asilimia 30 ya pato hilo. Tanzania inakisiwa kuwa na asilimia 1.4 ya idadi ya ng'ombe wote duniani na asilimia 11 barani Afrika, ikiwa ya pili kwa kuwa na ng'ombe wengi huku Ethiopia ikiongoza.

  Tanzania ina takriban ng'ombe 30.5 milioni, mbuzi 18 milioni, kondoo 5.3 milioni. Mifugo mingine ni pamoja na nguruwe, kuku wa kienyeji na kuku wa kisasa.

  Sekta ya mifugo imeajiri asilimia 50 ya wadau ikijumuisha wa moja kwa moja na kwa njia mbadala wanaofikia milioni 4.6.

  Hata hivyo, utajiri huo bado haujawakomboa Watanzania wengi hususani wafugaji kwa kukabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile uduni wa teknolojia ya kijenetiki, ukosefu wa malisho, magonjwa na ukosefu wa viwanda vya kuongeza thamani.

  Wafugaji wenye makundi makubwa ya mifugo wamekuwa wakihamahama ili kutafuta malisho, jambo linalosababisha migogoro ya ardhi sehemu mbalimbali nchini.

  Kutokana na ukame na kukosekana maeneo rasmi ya malisho, mifugo imekuwa ikifa kwa kukosa maji na malisho bora.

  Kutokana na hali hiyo, Serikali imekuja na Mpango Kabambe wa Mifugo Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa uchambuzi wa sekta ya mifugo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako