• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Simba yawaangusha wababe AS Vita na kufuzu robo fainali klabu bingwa Afrika

  (GMT+08:00) 2019-03-18 09:12:16

  Rekodi ya kwanza imewekwa juzi Jumamosi katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na timu ya Simba kutoka Tanzania imekuwa timu pekee kutoka Afrika Mashariki iliyofuzu kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kushika nafasi ya pili katika hatua ya makundi.

  Simba ilishika nafasi ya pili kwenye kundi D baada ya kujikusanyia alama 9 katika mechi 6 zikiwemo 3 zilizotokana na ushindi wa magoli 2-1 kwenye mechi ya mwisho dhidi ya AS Vita ya DRC uliopigwa mjini Dar es Salaam.

  Goli la kwanza la simba kwenye mechi hiyo lilifungwa na Mohamed Hussein likiwa ni la kusawazisha baada ya AS Vita kufunga goli la mapema kupitia Francy Kazadi Kasengu, huku goli la ushindi la Simba likifungwa na Clatous Chama katika dakika ya 89, na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kama ambavyo mechi ilitangazwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC na kisha Rais wa TFF Wallace Karia alitoa maoni yake.

  Aidha katika kundi hilo timu nyingine iliyofuzu na kushika ya kwanza ni Al Ahly ya Misri iliyokusanya alama 10.

  AS Vita yenye alama 7 na JS Soura ya Algeria yenye alama 9 zimeshindwa kufuzu kutoka hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako