• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA NA KUOGELEA: Kenya yavuna medali za dhahabu mashindano ya Olimpiki kwa wenye ulemavu UAE

    (GMT+08:00) 2019-03-18 09:16:07

    Kenya imezoa medali mbili za dhahabu Jumamosi katika mashindano ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu yanayoendelea jijini Abu Dhabi katika Milki za Kiarabu. Medali ya kwanza ilipatikana katika fani ya bocce pale Wakenya Deepak Sanghvi, Effie Owuor, Marion Iravaya Obiri na Veer Rajesh walizoa dhahabu.

    Timu ya Kenya ilikamilisha mbele ya Mauritius, Oman, Romania na China Taipei.

    Kwa upande wa waogeleaji Faith Muchiri, Charlton Waithaka, Sonali Ritesh na Kagondu Kariuki wamenyakua nishani ya fedha katika kitengo cha 4×25 relay.

    Kenya inawakilishwa na wanamichezo 71 ikiwa Inashiriki kwenye michezo ya soka, mpira wa vikapu, voliboli, voliboli ya ufukweni, handiboli, riadha, bocce, kuendesha baiskeli, gofu, kuogelea kwenye bwawa na kuogelea katika mto, ziwa ama bahari (Open Water Swimming).

    Mashindano haya ya dunia yalianza rasmi Machi 14 yakihusisha zaidi ya mataifa 170 yatakamilika Machi 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako