• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kutatua mgogoro kati ya TRC na SBL

    (GMT+08:00) 2019-03-18 19:08:51

    Serikali imesema itatumia busara kumaliza mgogoro kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kiwanda cha Bia cha Serengeti (SBL) ulioibuka Septemba mwaka jana.

    SBL ni moja ya viwanda vikubwa vitatu vilivyopo mkoani Kilimanjaro pamoja na Bonite Bottlers (BBL) na Kiwanda cha Sukari (TPC).

    Mgogoro huo uliibuka baada ya TRC wakati huo ikijulikana kama kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco) kuweka alama ya kutaka kubomoa sehemu ya majengo ya kiwanda hicho.

    Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Bi Stela Manyanya amesema uwekezaji uliofanywa na SBL ni mkubwa na Serikali itatumia busara kuumaliza.

    Manyanya alifika kiwandani hapo akiwa amefuatana na wajumbe wa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Uongozi wa kiwanda hicho ulitumia nafasi hiyo kuomba mgogoro huo ufikishwe mwisho. Serikali imesema itatumia busara kumaliza mgogoro kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kiwanda cha Bia cha Serengeti (SBL) ulioibuka Septemba mwaka jana.

    SBL ni moja ya viwanda vikubwa vitatu vilivyopo mkoani Kilimanjaro pamoja na Bonite Bottlers (BBL) na Kiwanda cha Sukari (TPC).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako