• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mali ya Yusuph Manji yazuiwa na serikali ya Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-03-18 19:09:22

    Mahakama Kuu imezuia mali za mfanyabiashara maarufu nchini humo Yusuph Manji kutokana na madeni anayodaiwa na Benki ya NBC.

    Manji anadaiwa zaidi ya Sh25 bilioni na benki hiyo ambazo ameshindwa kuzirejesha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba, hivyo mali zake zilizopo Mwanza na Dar es Salaam ambazo ziliwekwa dhamana, kuzuiwa. Mali hizo zimezuiwa kwa oda mbili tofauti za mahakama hiyo zilizotolewa Februari 19 zinazomzuia Manji kufanya muamala wa aina yoyote kuzihusu ikiwamo kuhamisha umiliki kama zawadi, kuuza au kuweka dhamana. Oda ya kwanza inayotokana na kesi ya biashara namba 54 ya mwaka 2018 inaizuia kampuni ya Manji Tanperch kufanya chochote kwenye kitalu namba 8, 9 na 127 vilivyopo eneo la viwanda Ilemela kwa jina la Tanperch Limited kwa kushindwa kulipa deni la Sh18.7 bilioni kutoka Benki ya NBC. NBC ilifingua kesi mwaka 2016 ikizishtaki kampuni za Farm Equip (T) Limited, Tanperch Limited na Quality Group Limited zinazomilikiwa na Kaniz Manji na Yusuf Manji kwa kushindwa kurejesha Sh15.9 bilioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako