• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa wito wa kuijengea DRC uwezo wa kujilinda usalama

    (GMT+08:00) 2019-03-19 08:20:50

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa mataifa Balozi Wu Haitao ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kujenga uwezo wake wa kulinda usalama.

    Balozi Wu Haitao ameliambia Baraza la usalama kwenye mkutano kuhusu hali ya nchini DRC, kuwa kipaumbele kwa sasa kinatakiwa kuwa kuisaidia nchi hiyo kuimarisha uwezo wake wa kulinda usalama na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya DRC, katika kudumisha amani na utulivu nchini humo.

    Balozi Wu amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu kikamilifu mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi wa DRC, na pia inatakiwa kuheshimu kikamilifu uongozi wa serikali ya DRC katika kushughulikia mambo yake ya ndani, kuimarisha mawasiliano na serikali ya DRC na kuisaidia kutatua changamoto zinazoikabili kwenye masuala ya kibinadamu, usalama, maendeleo na mengineyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako