• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais wa China barani Ulaya kuanzisha "wakati wa mafanikio" wa uhusiano kati ya pande hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-03-19 16:50:42

    Rais Xi Jinping wa China Alhamisi ataanza ziara rasmi katika nchi tatu za Ulaya, Italia, Monaco na Ufaransa. Wachambuzi wanaona si hali ya kawaida kwa kiongozi wa China kuchagua Ulaya kufanya ziara yake ya kwanza kwa mwaka huu, na pande hizo mbili zinatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu masuala muhimu yakiwemo uhusiano wa kibiashara, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mawasiliano kati ya staarabu.

    Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi amesema, bila kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa, China itaweka kipaumbele katika uhusiano kati yake na Ulaya, na ziara ya rais Xi itaanzisha "wakati wa mafanikio" wa uhusiano huo.

    Chanzo cha kwanza cha "wakati wa Mafanikio" wa uhusiano kati ya China na Ulaya ni uongozi wa kimkakati wa viongozi wa pande hizo mbili. Miaka mitano iliyopita, rais Xi akifanya ziara barani Ulaya alisema, inapaswa kufikiria uhusiano kati ya China na Ulaya kwa mtizamo wa kimkakati, na kuunganisha nguvu, masoko na ustaarabu wa pande hizo mbili, ili kuanzisha uhusiano wa kiwenzi katika shughuli za amani, ongezeko la uchumi, mageuzi na ustaarabu.

    Chanzo cha pili cha "wakati wa Mafanikio" wa uhusiano kati ya China na Ulaya ni kwamba China na nchi za Ulaya zenye mifumo tofauti ya kisiasa siku zote zinajitahidi kuendeleza uhusiano wa kirafiki. China na nchi za Ulaya zina utamaduni na mifumo tofauti, na pia ziko katika vipindi tofauti vya maendeleo, lakini hali hii haizuii pande hizo mbili kuendeleza ushirikiano wao. China na Ulaya ni wenzi wakubwa wa kibiashara, katika miezi miwili iliyopita, thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia dola bilioni 110 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 8.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

    Chanzo cha tatu cha "wakati wa Mafanikio" wa uhusiano kati ya China na Ulaya, ni kwamba pande hizo mbili zinahitajika kutoa mchango katika kutuliza hali tatanishi ya kimataifa kwa kuhimiza mshikamano na uaminifu. Mwaka huu hali ya kimataifa haswa barani Ulaya bado ina utatanishi, wakati vitendo vya upande mmoja, kujilinda kibiashara, kufuata maoni ya umma na ugaidi vinaongezeka, uchaguzi wa Umoja wa Ulaya utafanyika. Ziara ya rais Xi si kama tu itahimiza kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mkakati wa Umoja wa Ulaya wa kuwasiliana zaidi na Asia, na kutoa nguvu mpya kwa ajili ya maendeleo endelevu ya uchumi wa dunia, bali pia itahamasisha nchi mbalimbali za Ulaya kukaa pamoja kwa urafiki na kushirikiana vizuri ili kupata mafanikio ya pamoja.

    Miaka mitano iliyopita, rais Xi akihutubia barani Ulaya alisema, sababu ya kuelewana vibaya ni kutengana, na mawasiliano yanaweza "kuwasha taa ya busara". Inatarajiwa kuwa "wakati wa mafanikio" wa uhusiano kati ya China na Ulaya utawasha "taa ya busara", na kuleta mwanga zaidi kwa dunia hii yenye hali yenye utatanishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako