• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa majeshi ya Syria, Iran na Iraq wakutana nchini Syria

    (GMT+08:00) 2019-03-19 19:22:13

    Waziri wa ulinzi wa Syria Jenerali Ali Abdallah Ayyub, mnadhimu mkuu wa jeshi la Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri na mnadhimu mkuu wa jeshi la serikali ya Iraq Bw. Othman al-Ghanmi wamekutana jana mjini Damascus, Syria, na kujadiliana kuhusu ushirikiano katika kupambana na ugaidi, kufungua mipaka na maendeleo ya hali ya Syria.

    Jenerali Ayyub amesema, wapiganaji wa kundi la Kikurdi wanakabiliwa na machaguo mawili, kufikia maafikiano au kuchukuliwa kinguvu eneo linalodhibitiwa na kundi hilo. Pia amesema serikali ya Syria itarudisha uthibiti wa maeneo yote ya Syria.

    Meja Jenerali Bagheri amesema, nchi hizo tatu zilijadiliana suala la kufungua kituo cha mpaka kati ya Iraq na Syria na pia nchi hizo zitafanya mawasiliano katika suala la kupambana na kundi lenye msimamo mkali la Islamic State.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako