• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Waliolipwa korosho kuwekwa wazi

  (GMT+08:00) 2019-03-19 20:03:01
  Baada ya baadhi ya wakulima wa korosho kulalamika kutolipwa msimu huu, Serikali imesema itabandika majina ya wote walioingiziwa fedha kwenye akaunti zao kila kijiji.

  Kutokana na madai hayo kuibuka sintofahamu, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema njia ya kumaliza mzizi wa fitina umepatikana na sasa kila kitu kitakuwa bayana.

  Hasunga alisema hayo jana alipozungumza na Kamati ya Bunge ya Mifugo na Maji katika ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.

  Waziri Hasunga alisema tayari tani 222,684 zimekusanywa hadi Machi 14 na Sh596.9 bilioni zimelipwa kwa wakulima sawa na asilimia 83 ya Sh723 bilioni zinazotakiwa kulipwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako