• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Uwanja wa ndege wa Lindi wakamilika asilimia 75

    (GMT+08:00) 2019-03-19 20:03:17
    Kazi ya ukarabati wa mradi wa kiwanja cha ndege kilichopo wilayani Nachingwea, mkoani Lindi Tanzania, wenye thamani ya Sh. milioni 943 umefikia asilimia 75.

    Mkandarasi wa mradi huo ambaye ni Kampuni ya Makapo Construction Ltd amesema amefikia hatua ya G-15.

    Utekelezaji wa ukarabati wa kiwanja hicho ni miongoni mwa mpango mkakati wa serikali katika kuboresha viwanja vya ndege nchini ili kuongeza thamani na tija kwenye usafiri wa anga nchini.

    Injinia Mkuu wa ujenzi huo, Helifuraha Hema, alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa waandishi wa habari waliotembelea kiwanja hicho kuangalia maendeleo ya ujenzi.

    Alisema serikali imetoa Sh. milioni 943 kwa ajili ya kufanya ukarabati wa kiwanja ndege cha Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni miongoni mwa mkakati wa kuboresha viwanja vyote vya ndege nchini ili kuboresha usafiri wa anga nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako