• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia chafanana na ajali ya Indonesia

  (GMT+08:00) 2019-03-19 20:14:19

  Ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi wa usalama wa ndege ya nchini Ufaransa imesema, chanzo cha ajali ya ndege ya Boeing ya kampuni ya ndege ya Ethiopia kinafanana na ajali ya ndege ya Boeing ya kampuni ya ndege ya Lion ya Indonesia.

  Ripoti hiyo imesema, idara ya uchunguzi wa ajali ya Ethiopia, kamati ya usalama wa usafiri ya Marekani na taasisi hiyo vitathibitisha chanzo hicho kwa kutumia visanduku vyeusi viwili.

  Hivi sasa, data za visanduku hivyo zimekabidhiwa kwa idara ya uchunguzi wa ajali ya Ethiopia ambayo itatoa ripoti ndani ya siku 30.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako