• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Syria na waziri wa ulinzi wa Russia wajadili suala la Idlib na mkoa wa Euphrates

    (GMT+08:00) 2019-03-20 10:10:37

    Shirika la habari la serikali la SANA la Syria limesema rais Bashar al-Assad wa Syria amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Russia Bw. Sergey Shoygu na kujadiliana naye kuhusu hali ya jimbo la Euphrates lililoko Mashariki ya Syria na mkoa wa Idlib.

    Pande hizo mbili zimekubali kuendelea kushirikiana ili kupata ufumbuzi unaofaa kwa masuala ya Idlib, ambayo ni ngome ya mwisho ya waasi wa Syria, na eneo la mashariki ya Mto wa Euphrates, ambalo kwa kiasi kikubwa linadhibitiwa na kundi la SDF linaloungwa mkono na Marekani.

    Bw. Assad na Bw. Shoygu pia wamejadili ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika jitihada za kupambana na ugaidi na mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na makundi ya IS na kundi la Nusra Front lenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako