• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huu ni mwaka muhimu kwa China kushinda vita dhidi ya umaskini

    (GMT+08:00) 2019-03-20 16:56:43

    Mikutano ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China iliyofungwa wiki iliyopita imedhihirisha majukumu mapya ya mwaka huu ya watu wa China. Kati ya majukumu hayo, kushinda vita dhidi ya umaskini ni muhimu sana. Wakati wa mikutano hiyo, rais Xi Jinping alitaja suala la umaskini mara nyingi, na kusisitiza kuwa imebaki miaka mwili tu kabla ya kufikia mwaka 2020, ambao ni mwaka wa kutimiza lengo la kuondoa umaskini nchini China, hivyo sasa ni wakati muhimu, na inapaswa kufanya juhudi kadiri iwezekanavyo hadi kupata ushindi wa mwisho.

    China imepata mafanikio dhahiri katika kupunguza umaskini ambao ni changamoto kubwa zaidi inayokabili dunia nzima. Takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 1978 hadi 2017, China ilipunguza idadi ya watu maskini kwa zaidi ya watu milioni 700, ambao ni asilimia 70 ya watu wote walioondokana na umaskini duniani.

    Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali za kihistoria na kimaendeleo, bado kuna mamilioni ya watu maskini nchini China. Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, bado kulikuwa na watu maskini milioni 16.6 vijijini, China. Serikali imeahidi kuwasaidia watu milioni 10 kuondokana na umaskini mwaka huu. Ahadi hiyo ni muhimu sana kwa China kutimiza lengo la kuondoa umaskini na kujenga jamii yenye maisha bora kabla ya mwaka 2020.

    Ili kushinda vita dhidi ya umaskini, China itachukua hatua sita muhimu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama wa chakula, kuhimiza mageuzi ya muundo wa uzalishaji wa kilimo, kujenga mwamko wa uhifadhi wa mazingira, kuendeleza miundombinu vijijini, kuimarisha shughuli za vijijini, na kuhimiza mageuzi. Aidha, mwaka huu serikali ya China itaunganisha mipango ya kupunguza umaskini na kustawisha vijiji, na kuwasaidia watu kuondokana na umaskini, kupitia kuendeleza sekta za uchumi vijijini.

    Ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, China imepata mafanikio makubwa katika kupunguza umaskini, huku ikiendelea na juhudi za kutokomeza umaskini. Juhudi hizo ni mchango wa China kwa dunia nzima, na pia ni utekelezaji wa mawazo ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

    Rais Xi alihutubia kongamano la ngazi ya juu la mwaka 2015 la kupunguza umaskini, akipendekeza kuharakisha mchakato wa kupunguza umaskini duniani. Alisema miaka 15 ijayo ni kipindi muhimu kwa nchi zinazoendelea ikiwemo China kupata maendeleo, China itashirikiana na pande nyingine kuboresha uhusiano wa wenzi wa kimaendeleo, na kuhimiza ushirikiano kati ya nchi za kusini, na ushirikiano kati ya nchi za kusini na kaskazini, ili kutoa rasilimali na nguvu kubwa kwa ajili ya juhudi za kupunguza umaskini duniani. Mikutano ya mwaka huu ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ilitambulisha dunia tena kuhusu nia, majukumu na hatua halisi za China katika kuondoa umaskini. Kushinda vita dhidi ya umaskini si kama tu ni utekelezaji wa ahadi ya China kwa wananchi wake, bali pia ni mchango mpya wa China kwa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako