• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gesi yakosekana Lamu

    (GMT+08:00) 2019-03-20 18:37:59

    Shughuli ya kuchimba gesi ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda wa mwaka mmoja uliopita katika kisiwa cha Pate, Kaunti ya Lamu hatimaye imekamilika, huku gesi ikikosekana.

    Shughuli hiyo iliyong'oa nanga rasmi Aprili. 2018 imekuwa ikitekelezwa na kampuni ya Zarara Oil and Gas Limited.

    Mkurugenzi wa Kampuni hiyo nchini Kenya, Peter Nduru, alisema jumla ya mita 4,307 zilichimbwa kwenda chini katika kisiwa cha Pate-2 lakini hadhi ya gesi iliyokuwa ikitafutwa ikakosekana.

    Bw Nduru alisema shughuli ya kutafuta gesi hiyo ambayo ilifaa kukamilika tangu Oktoba 2018 ilichukua muda mrefu kutokana na changamoto za mawe magumu ambayo yalikuwa yakivunjwa wakati wa shughuli ya uchimbaji na utafutaji wa gesi hiyo ilipokuwa ikitekelezwa.

    Pia kiwango cha juu cha presha ambayo ilipatikana eneo husika ni kiini cha shughuli ya kuchimba na kusaka gesi hiyo kuchukua muda mrefu kinyume na ilivyopangwa awali. Shughuli ya kuchimba madini hayo ilijiri miaka 48 baadaye kufuatia majaribio yaliyotekelezwa na kampuni ya Shell-BP mnamo 1971, ambapo kisima cha kwanza cha Pate 1 kilichimbwa na madini ya gesi na mafuta kugunduliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako