• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nairobi ndio mji ghali zaidi kuishi

  (GMT+08:00) 2019-03-20 18:39:28

  Utafiti ulifanywa unaonesha kuwa mji wa Nairobi kuwa ghali zaidi kuishi ukilinganishwa na miji mingine barani Afrika.

  Ripoti hiyo iliyofanywa na shirika la Economist Intelligence Unit Worlwide Cost of Living inasema gharama ya maisha mjini Nairobi imeongezeka katika maeneo 13 ikilinganishwa na mwaka jana na kuiweka Nairobi kuwa ya 63 kote duniani.

  Mji wa Lagos Nigeria unashikilia nafasi ya 127 duniani ukiwa ni wa kumi duniani miongoni mwa nchi zenye gharama ya chini zaidi kuishi. Utafiti huo ulifanywa kwa watu zaidi ya elfu 50 wakilinganishwa na bidhaa 160 pamoja na huduma.Utafiti huo uliangalia bei ya chakula, vinywaji, mavazi, vifaa vya nyumbani na mahitaji ya kibinafsi ukilinganisha na watu hao elfu 50.Mara nyingi ripoti hiyo hutumiwa na makampuni kuangalia gharama ya maisha na jinsi watakavyoweka bei kwa bidhaa zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako