• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msumbiji yafanya maombolezo ya siku tatu kwa watu waliofariki kutokana na kimbunga Idai

    (GMT+08:00) 2019-03-20 18:49:50

    Serikali ya Msumbiji imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo kwa wahanga wa kimbunga Idai kilichosababisha mvua kubwa na mafuriko katika mkoa wa Sofala ulioko katikati mwa nchi hiyo.

    Rais Felipe Nyusi wa nchi hiyo ametangaza hivyo baada ya kukutana na Baraza lake la Mawaziri jana usiku katika mji wa Beira ambao umeathirika zaidi na kimbunga hicho kilichotokea alhamis iliyopita. Rais Nyusi amesema, katika siku hizo za maombolezo, bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti nchini humo na katika balozi za nchi hiyo.

    Wakati huohuo, Ubalozi wa China na Jumuiya ya Wachina nchini Zimbabwe imetoa msaada wa chakula, maji safi ya kunywa na vifaa nyenye thamani ya dola za kimarekani laki 2, huku Ubalozi wa Marekani ukitoa mchango wa dola za kimarekani elfu moja kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo.

    Umoja wa Ulaya nao umetoa msaada wa dharura kwa Msumbiji, Malawi na Zimbabwe wenye thamani ya Euro milioni 3.4 kusaidia kukabiliana na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Idao kwenye nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako