• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China kufanya ziara yake ya kwanza kwa mwaka huu nchini Italia

    (GMT+08:00) 2019-03-20 19:46:45

    Rais Xi Jinping wa China kesho ataanza ziara rasmi katika nchi tatu za Ulaya, na Italia ni kituo chake cha kwanza.

    Kabla ya ziara hiyo, rais Xi ametoa makala kwenye Gazeti la II Corriere Della Sera la Italia, akisema mawasiliano ya miaka zaidi ya elfu mbili kati ya China na Italia yameleta mawazo yao ya pamoja ya kuheshimiana, kujifunzana, kuaminiana na kuelewana, na kuwa uhakikisho wa maendeleo ya urafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Huu ni mwaka wa 15 tangu China na Italia zianzishe uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote, na ziara ya rais Xi nchini Italia ina maana ya kihistoria kwa kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Inatarajiwa kuwa pande hizo mbili zitaimarisha ushirikiano katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kufikia makubaliano katika sekta za diplomasia, biashara, utamaduni, miundombinu, na fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako