• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Droo ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho yafanyika, makundi yajulikana

  (GMT+08:00) 2019-03-21 10:15:41

  Upangaji ratiba wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika umekamilika huku mabingwa wa Tanzania, Simba Sports Club wakirudishwa nchini DRC tena safari hii kuvaana na TP Mazembe.

  Simba itaanzia nyumbani Dar Es Salaam kutokana na mfumo wa michuano hiyo kwakuwa walimaliza wakiwa nafasi ya pili katika kundi D. Mchezo wa kwanza wa Simba na TP Mazembe utapigwa kati ya April 5 au 6 jijini Dar es Salaam na marudiano kati ya April 12 na 13 mjini Lubumbashi DRC.

  Wana wengine wa Afrika Mashariki, Gor Mahia ya Kenya wao watavaana na Berkane kutoka nchini Morocco.

  Michezo ya nusu fainali ya kombe la shirikisho itachezwa Aprili 28 na marudiano Mei 5 huku fainali ya kwanza ya kombe la Shirikisho msimu wa 2018-2019 itachezwa Mei 19 na marudiano yatakuwa Mei 26.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako