• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya ngazi ya juu ya biashara kati ya China na Marekani kufanyika hivi karibuni mjini Beijing na Washington kwa nyakati tofauti

    (GMT+08:00) 2019-03-21 17:14:32

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo amesema, naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni kiongozi wa China katika mazungumzo ya uchumi kati ya China na Marekani Bw. Liu He na mjumbe wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer pamoja na waziri wa mambo ya fedha wa nchi hiyo Bw. Steven Mnuchin hivi karibuni wamefanya mazungumzo kadhaa kwa njia ya simu.

    Amesema pande mbili hizo zimekubaliana kuwa, Bw. Lighthizer na Bw. Mnuchin watafanya ziara nchini China wiki ijayo na kushiriki kwenye duru ya nane ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya biashara kati ya China na Marekani.

    Bw. Liu atafanya ziara nchini Marekani mwanzoni mwa Aprili na kushiriki duru ya tisa ya mazungumzo kama hayo yatakayofanyika mjini Washington.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako